Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, Ayatullah Jawadi Amuli katika ujumbe wa video uliotolewa kutokana na mnasaba wa kuanza mwaka mpya wa masomo wa Hawza ya mji wa Amol Iran, huku akiwapongeza na kuwakaribisha wanazuoni, wasomi na wanafunzi wa Hawza, alisisitiza umuhimu wa kuifahamu hakika ya elimu, mwanadamu na njia ya mwanadamu kufikia elimu.
Akieleza kwamba “thamani ya elimu inategemea kile kinachojulikana, na thamani ya mwenye elimu inategemea elimu,” aliitaja elimu kuwa miongoni mwa nguzo muhimu za mfumo wa uumbaji, na kwa kurejelea Aya za Qur’ani Tukufu akasema: Mwenyezi Mungu Mtukufu mwenyewe amejitambulisha kuwa ni Mwalimu, na akamfundusha mwanadamu wa kwanza pale aliposema:
﴿وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ کُلَّهَا﴾
“Na akamfundisha Adam majina yote.”
Kisha akasema:
b
“Amemfundisha mwanadamu yale ambayo hakuwa anayajua.”
Mwenyezi Mungu alianza uumbaji na uwepo wa mfumo wa elimu, anaendelea kuuendesha kwa elimu, na atauhitimisha kwa elimu.
Mtukufu huyo, huku akisisitiza uhusiano wa kina uliopo baina ya elimu na rehema, alirejelea Aya za Sura Tukufu ya Ar-Rahman na kusema:
Yaani, njia ya mafundisho ya Mwenyezi Mungu huanza kwa rehema, huendelea kwa kufundishwa Qur’ani, humfikisha mwanadamu katika kuwa mwanadamu, na hatimaye humfikisha katika uwezo wa kujieleza. Yaani: “الرحمن” ni ya kwanza, “علم القرآن” ni ya pili, baada ya hayo “خلق الإنسان” ni ya tatu, na kisha “علمه البيان” ni ya nne.
Alisisitiza kwamba kile kinachotoka katika ulimi na kalamu ya mwanadamu huwa ni “bayān” (maelezo/ufafanuzi) pale tu kinapotoka kwa mwanadamu ambaye ni mwanafunzi wa Qur’ani na aliyeelimishwa na mafundisho ya Mwenyezi Mungu; si kutoka kwa mtu ambaye maneno na maandishi yake yametokana na matamanio, hawaa na matakwa ya nafsi.
Mtukufu huyo alisisitiza: Nguzo nne zinazojadiliwa katika Hawza na vyuo vikuu ya kwanza ni Tawhidi, kisha kufundishwa Qur’ani, halafu kuwa mwanadamu, na baada ya hapo kuzungumza, kufundisha na kulea.
Ayatullah Jawadi Amuli, katika sehemu nyingine ya hotuba yake, huku akirejelea kauli ya Amirul-Muuminina (a.s) kuhusu elimu na imani, alisisitiza umuhimu wa kuunganisha elimu na imani, na kusema:
«بِالْإِیمَانِ یُعْمَرُ الْعِلْمُ»
“Kwa imani, elimu hujengwa.”
Elimu wakati mwingine huchakaa na kupitwa na wakati, na kinachoitengeneza, kuihuisha na kuifanya iwe na matokeo ni imani. Ni imani inayoiweka elimu ikiwa hai, changamfu na yenye kuzaa matunda.
Akieleza kwamba elimu iliyochakaa haiwezi kuzaa jamii iliyostaarabika, aliongeza: Hawza inaweza kuwa imejengwa vizuri na kuijenga jamii ikiwa elimu yake, pamoja na kuwa hai, pia ni yenye afya na iliyojengwa vizuri; na ujenzi na ustawi wa elimu unatokana na imani.
Iwapo mtu ameifahamu njia yake, akaifuata njia yake, na hakumzuia mwingine kufuata njia yake, basi elimu hii ni “ma‘mur”, yaani imejengwa na kustawi. Hawza iliyojengwa vizuri huijenga jamii; chuo kikuu kilichojengwa vizuri huijenga jamii.
Hapo hakutakuwa tena na vita. Hakutakuwa tena na uvamizi wa yale madola mawili yenye nguvu na tabia za kishetani. Hakuna mtu atakayekwenda katika njia isiyo sahihi, wala hakuna mtu atakayemzuia mwingine kufuata njia yake.
Mtukufu huyo, huku akisisitiza umuhimu wa kufikia elimu mpya na yenye afya, alibainisha: Elimu ambayo imepitwa na wakati na kuchakaa, haiwezi kuipeleka Hawza katika ustawi wala kukifanya chuo kikuu kuwa chenye hadhi na utukufu. Kwa hiyo, ni lazima kujifunza elimu ambayo haitachakaa; na endapo dalili za kuchakaa zitatokea ndani yake, basi inapaswa kurekebishwa kwa imani na matendo mema.
Akiziombea mafanikio Hawza na vyuo vikuu, alieleza matumaini yake kwamba: Hawza yetu iwe Hawza ambayo “بالایمان یعمر العلم”, yaani “kwa imani elimu hujengwa,” na chuo chetu kikuu pia kiwe chuo ambacho “بالایمان یعمر العلم”, yaani “kwa imani elimu hujengwa.”
Ayatullah Jawadi Amuli pia alimuomba Mwenyezi Mungu awape heshima na ushindi watu wa Iran, auhifadhi na kuuimarisha mfumo wa Kiislamu, na awape mafanikio wanazuoni, wanafunzi wa Hawza na wote wanaoihudumia dini na jamii.
Aidha, alieleza matumaini yake kwamba jamii ya Kiislamu itabadilika na kuwa jamii ya Alawi, na kwamba mfumo huu utakabidhiwa mikononi mwa mwenyewe na mmiliki wake halisi, yaani Imam wa Zama, Mtukufu Waliyul-Asr (Mwenyezi Mungu aharakishe kudhihiri kwake).
Maoni yako